Machapisho

AJALI YA TRENI DODOMA

Treni ya abiria iliyokua inatokea Dar es salaam kuelekea Bara (Mwanza,Mpanda na Kigoma kupitia Tabora)Imepata ajali Wilayani Bahi umbali wa KM 40 kutoka Dodoma,Mkurugenzi mkuu wa shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amethibitisha. "Treni ilikua na zaidi ya watu 700,kuna mvua zinanyesha sana bado hatujajua chanzo cha ajali,ila kichwa kimeanguka,Taarifa za awali zinaonesha mfanyakazi wetu mmoja amefariki Na abiria wawili wamefariki, Nilikua likizo lakini nimeikatisha naelekea eneo la tukio"